Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Mnamo mwaka wa 2017 tarehe 21 mwezi wa 11 Rais Robert Mugabe aliamua kujiuzulu na kuachia madaraka ya kuwa Rais wa Zimbabwe baada ya kutawala taifa hilo kwa miaka 37

November 20, 2018

Robert Gabriel Mugabe  amezaliwa  tarehe  21 Februari 1924 amekuwa kiongozi wa Zimbabwe tangu 1980. Yeye ni mwenyekiti wa chama tawala cha ZANU.

1980 alikuwa waziri mkuu na 1987 Rais wa Zimbabwe. Kabla ya wakati ule aliongoza upinzani wa ZANU dhidi ya serikali ya walowezi Waingereza nchini waliofuata siasa ya ubaguzi wa rangi.

Mugabe aliendelea   kushiriki katika uchaguzi mbalimbali nchini zimbabwe. Tangu mwaka 2000  chaguzi zote zilikuwa mashakani kutokana na matishio na matumizi ya mabavu dhidi ya wapinzani.

 

Utawala wa Mugabe uliitwa wa kidikteta tangu mwaka 2002. Kutokana na mashataka dhidi ya serikali ya Mugabe ya kudharau haki za binadamu nchini humo ilisimamishwa ndani ya Jumuiya ya Madola.

 

Mugabe pamoja na mawaziri wake na viongozi wa chama chake hawakuruhusiwa kusafiri kwenda nchi za Umoja wa Ulaya na Marekani.

Mwanzoni  mwa  utawala wake Mugabe alisifiwa kujenga uchumi na sera ya elimu nchini.

Zimbabwe ilikuwa nchi iliyouza vyakula vingi nje. Tangu mwanzo wa milenia mpya pamoja na mashtaka ya udikteta hali ya uchumi ilirudi nyuma.

Takriban milioni mbili za raia wa Zimbabwe walioondoka nchini  zimbabwe wakikaa kama wakimbizi Afrika Kusini

 

TUHUMA ZA MAUAJI NA UKANDAMIZAJI

 

Baada tu ya kushika madaraka, Mugabe aliamua kuimarisha jeshi lake la kumlinda (liitwalo Gukurahundi) ambalo lilijengwa na watu kutoka kabila lake la wa-Shona.

 

Nchi hiyo ilikuwa tayari imegawanyika kikabila hata katika uchaguzi wa kwanza wa 1980, washona wote walimchagua Mugabe na Wa-Ndebele na wabunge kutoka chama cha ZANU. Wakati wandebele walichagua viongozi kutoka chama cha ZAPU kilichoongozwa na Joshua Nkomo.

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload