Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 19.11.2018: Fabregas, Pellegrini, Arnautovic, Bale, Benzema, Umtiti

November 19, 2018

AC Milan wameanza mazungumzo ya kusaini kiungo wa kati wa Uhispania Cesc Fabregas, 31, kutoka Chelsea. (Calciomercato).

 

Manchester United wako tayari kuongeza maradufu mshahara wa kiungo wa kati wa Roma raia wa Italia mwenye miaka 22 Lorenzo Pellegrini, ambaye amehusishwa na kuhama kwenda Old Trafford kwa pauni milioni 26. (Corriere dello Sport, via Football Italia)

 Real Madrid wako tayari kumsaini mshambulizi mwezi Januari baada ya kupoteza imani yao kwa raia wa Wales Gareth Bale na mfaransa Karim Benzema,30. 

 

Barcelona huenda wakamsaini mlinzi wa kati mwezi Januari kwa sababu ya wasi wasi kihusu hali ya kiafya ya mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa Samuel Umtiti, 25.

Mshambuliaji wa West Ham Marko Arnautovic, 29, hawawezi kusikiliza uvumi unaohusu kuhama kwake.

 

Mmiliki wa Newcastle United Mike Ashley ametafuta pesa za kununua wachezaji mwezi Januari.

 

Wachezaji wa zamani nwa Ligi ya Premier Ian Write na Robbie Savage wanaunga mkono uasi wa wachezaji 300 dhidi ya mkuu wa chama cha wachezaji kandanda wa kulipwa Gordon Taylor.

 

Meneja wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger anasema ni baada ya muda tu kabla ya kura za twitter zitaanza kutumiwa kwa mabadiliko ya wachezaji uwanjani wakati wa mechi

Manchester United itatoa ofa ya pauni ya milioni 60 kwa akipa wa Everton wa miaka 24 Jordan Pickford ikiwa Mhispania David de Gea, 28, hatakubali kuongeza mkataba wake. (Sun on Sunday)

Manchester City wamewashinda Barcelona katika mbio za kumsaini kiungo wa kati wa Ajax raia wa uholanzi mweye miaka 21 Frenkie de Jong

 

Liverpool wanatarajiwa kumsaini kiungo wa kati wa Hoffenheim Mjerumani Kerem Demirbay, 25, mwezi Januari (Sunday Express)

 

Lakini matumaini ya Liverpool kumsaini mlinzi wa Ajax anayewekewa thamani ya pauni milioni 60 Matthijs de Ligt yanaaonekana kufifia baada ya mchezaji huyo wa miaka 19 raia wa uholanzi kuhusishwa na Barcelona. (Sunday Mirror)

Paris St-Germain wamejiunga kwenye mbio za Arsenal na Tottenham kumwinda mlinzi wa Manchester United mwenye miaka 24 raia wa Ivory Coast Eric Bailly. (Mail on Sunday)

 

Kiungo wa kati wa Arsenal na wales Aaron Ramsey, 27, atalipwa pauni milioni 10.4 ikiwa atahama kwenda Juventus. (Sun on Sunday)

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload