Mwanamuziki kutoka nchini Marekani anayefahamika kwa jina la fabolous alizaliwa tarehe 18 mwezi wa 11 mwaka 1977

November 19, 2018

John David Jackson [fabolous]  (amezaliwa tar. 18 Novemba 1977) ni msanii wa rekodi za hip hop kutoka nchini Marekani.

Anafahamika zaidi kwa jina la kisanii kama Fabolous. Alikulia mjini Brooklyn huko New York City, alikuwa mmoja kati marapa wa East Coast ambao waliathiriwa na muziki wa Southern hip hop.

 

Moja kati ya kazi zake za awali ambayo ilimletea umaarufu ni pamoja na "Can't Deny It" mnamo 2001, kutoka katika albamu yake ya kwanza ya Ghetto Fabolous. Fabolous ametoa albamu tano, ambazo zote kwa ujumla zimeuza nakala zaidi ya milioni tatu huko nchini Marekani.

MAISHA NA KAZI..

 

Maisha ya awali na Mwanzo wa kazi

 

Fabolous anaitwa John David Jackson mnamo tar. 18 Novemba 1977 alizaliwa , na wazazi wenye asili ya Kiafrika-Kiamerika na Kidominika. Alikulia huko Bedford-Stuyvesant jirani kidogo na Brooklyn, New York. 

Wakati anasoma elimu ya juu, Fabolous akaanza kujifua katika masuala ya muziki wa rap. Alialikwa kurap moja kwa moja kipindi cha redio cha DJ Clue na kwenye WQHT Hot 97, ambapo kulimpatia uwezo wa kuweza kuingia mkataba na studio ya Desert Storm Records. Alipata kushirikishwa kwenye mamixi tepu kibao ya DJ Clue na mamixi tepu mengine mingi tu ya wasaniii wa Roc-A-Fella.

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon