Mnamo mwaka wa 1993 tarehe 18 mwezi wa 11 nchini Afrika kusini; vyama vya kisiasa 21 nchini humo vilipitisha katiba mpya iliyoruhusu kuwepo kwa uhuru wa kupiga kura kwa watu weusi na kufuta sheria zilizokuwa zinawapendelea watu weupe.

November 19, 2018

Afrika Kusini ni nchi kubwa katika Afrika  yenye wakazi takriban milioni 54.

Imepakana na Namibia, BotswanaZimbabweMsumbiji na Uswazi. Nchi nzima ya Lesotho iko ndani ya eneo la Afrika Kusini.

 

Mji mkubwa ni Johannesburg. Majukumu ya mji mkuu yamegawiwa kati ya miji mitatu: Cape Town ni makao ya Bunge, Pretoria ni makao ya Serikali na Bloemfontein ni makao ya Mahakama Kuu.

 JINA LA AFRIKA KUSINI

Nchi ina majina rasmi 11 kutokana na lugha rasmi 11, nazo ni: Kiafrikaans, Kiingereza, KizuluKixhosaKiswatiKindebeleKisotho cha Kusini, Kisotho cha KaskaziniKitsonga, Kitswana na Kivenda.

 

KOLONI LA WAHOLANZI

 

Chanzo cha Afrika Kusini kama nchi ni Koloni la Rasi iliyoundwa na Waholanzi katika eneo la Cape Town. Huko kabila jipya la Makaburu lilijitokeza kati ya walowezi Wazungu kutoka Uholanzi, Ufaransa na Ujerumani. Lugha yao ilikuwa Kiholanzi iliyoanza kuchukua maneno ya Kifaransa, Kiafrika na Kiingereza na kuendelea kuwa lugha ya pekee Kiafrikaans.

 

Karne za kwanza za koloni la Kiholanzi ziliona pia kufika kwa watumwa kutoka Indonesia walioletwa kama wafanyakazi wa Waholanzi na Makaburu. Hao Waindonesia walikuwa chanzo cha jumuiya ya Uislamu kwenye rasi.

 

Pia machotara walitokea kutokana na kuzaliana kati ya Makaburu na wanawake Waafrika na Waindonesia. Sehemu ya machotara hao wameingia katika jumuiya ya Makaburu na wengi wao wanapimwa kuwa na mababu Waafrika.

 

Katika miaka ya baadaye ubaguzi wa rangi uliongezeka na watoto machotara wa Wazungu na Waafrika mara nyingi hawakukubalika; walianza kuishi kama kundi la pekee kati ya Waafrika na Wazungu, nao ni chanzo cha hao walioitwa baadaye "Cape Coloreds".

 UBAGUZI WA RANGI

 

Ubaguzi wa rangi ni kitendo cha kuthamini au kutenga binadamu kwa misingi ya rangi za ngozi.

Ubaguzi wa rangi ulikuwa maarufu sana katika nchi kama Afrika Kusini kwa jina la "apartheid"  ambapo huko  South Afrika waafrika walikandamizwa kutokana na rangi yao katika kupata huduma mbalimbali za kijamii na kimaendeleo.

 

Wakati wa ukoloni, rangi ilitumika kama msingi wa utoaji huduma muhimu mfano: shule, matibabu na haki nyingine za kibinadamu. Rangi nyeusi ilipewa hadhi ya chini zaidi.

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon