katika nchi ya Misri tarehe 17 mwezi wa 11 mwaka 1869 mfereji wa suez unafunguliwa na kuunganishwa kwenye bahari ya Mediterranea pamoja na bahari nyekundu.

November 17, 2018

Mfereji wa Suez  ni mfereji mkubwa nchini Misri.

 

MAHALI PAKE

Unaunganisha Bahari ya Mediteranea na Bahari ya Shamu  na Bahari Hindi. Mfereji uko upande wa magharibi ya Rasi ya Sinai. Urefu wake ni 163 km na upana ni kuanzia 300m.

 

Unaanza mjini Port Said  upande wa Mediteranea na kuishia mjini Suez (al-Suways) upande wa Bahari ya Shamu.

 

HISTORIA YA MFEREJI WA SUEZ.

Ilijengwa kati ya 1859 na 1869 na kampuni ya kifaransa.

Kuna mifereji mbalimbali iliyotangulia hapa kuanzia karne ya 14 KK hadi wakati wa Waarabu katika karne ya 8 BK.

 

Lakini yote haikudumu kwa sababu ya matatizo ya kuondoa mchanga mara kwa mara kwa mitambo iliyopatikana zamani. Tena katika mifereji ya zamani ilikuwa serikali ya Misri tu iliyotaka kurahisisha usafiri na ubebaji wa mizigo.

 

Tangu kupatikana kwa meli ya kisasa idadi ya meli kati ya Ulaya na Asia iliongezeka sana katika karne ya 19. Zote zilipaswa kuzunguka Afrika yote au kuondoa mizigo na abiria upande wa mediteranea na kuyasafirisha yote hadi Suez. Hivyo ilikuwa jitihada ya kimataifa yaliyoleta mfereji wa kisasa.

Meli ya kwanza ilipita mfereji mpya tar. 17 Februari 1867. Mtungaji muziki Giuseppe Verdi aliandika opera yake Aida hasa kwa nafasi hii.

 

UMUHIMU WA MFEREJI  WA SUEZ

Mfereji umeharakisha na kurahisisha usafiri kati ya Ulaya, Asia na Afrika ya Mashariki. Zipatao meli 15,000 zinapita kwenye mfereji kila mwaka.

 

Mafanikio ya mfereji wa Suez yalihamasisha mianzo ya Mfereji wa Panama

 

KUTAIFISHWA  KWA MFEREJI 1956

 

Mfereji ulikuwa mali ya Compagnie universelle du canal maritime de Suez au Kampuni ya mfereji wa Suez na hisa zake zilikuwa mkononi mwa serikali za Ufaransa na Uingereza.

 

Mwaka 1956 serikali ya Misri chini ya rais Gamal Abdel Nasser ilitaifisha mfereji na tendo hili likasababisha vita ya Suez ya 1956 ambako Uingereza, Ufaransa na Israel zililazimishwa na mataifa makubwa kujiondoa katika Misri baada ya uvamizi wao.

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon