Mwanamziki wa kike kat deluna kutoka Marekani alizaliwa tarehe 17 mwezi wa 11 mwaka 1987

November 17, 2018

Kathleen Emperatriz "Kat" DeLuna  amezaliwa tar. 17 Novemba, mwaka 1987 mjini The Bronx, New York) lakini amekulia katika moja kati ya sehemu za Newark,  na New Jersey. Deluna  ni mwimbaji wa Kimarekani mwenye asili ya Kidominika.

 

Wazazi wake wote wanatokea huko Dominika, mama yake, ana miliki duka la mikate katika  mji wa Newark. Kwa sasa ameingia mkataba na studio ya Epic Records/GMB na studio ya Akon maarufu kama Konvict Muzik.

 

Konvict imetoa kile cha moyoni kwa kusema kuwa wanampango wa kuitoa upya albamu yake ya kwanza ya mwanadada huyu ya 9 Lives,

 

lakini maelezo yake ya hivi karibuni aliyoyatoa kupitia mtandao wa myspace na kusema kwamba, amerejea zake studio kwa ajili ya kutoa albamu ya pili, na kupendekeza kuwa albamu ya 9 Lives haito tolewa tena, bali atashughulikia albamu mpya tu.

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon