Stesheni ya Runinga ya Al Jazeera ilianzishwa Tarehe 15 november, mjini Doha huko Qatar na kua

Al Jazeera ilianzishwa mnamo 15 Novemba 2006. Stesheni hii ilikuwa iitwe Al Jazeera International lakini hili jina lilibadilishwa miezi tisa kabla ya uzinduzi.[siku kama ya leo mwezi kama wa leo lakini katika mwaka 2006 stesheni hii ilianzishwa mjini Doha]

Stesheni hii pia ililenga kufikia nyumba milioni 40, lakini ilipitisha lengo hili kwa kuweza kufikia nyumba milioni 80.

Al Jazeera English ni stesheni ya runinga ya kutangaza habari na taarifa za mambo leo masaa ishirini na nne kwa lugha ya Kiingereza iliyo na makao yake makuu ni mjini Doha, Qatar.

Stesheni hii huonyesha habari za makala na uchambuzi, mijadala, taarifa za mambo leo, biashara, teknolojia, na michezo. Wao hudai kuwa stesheni ya kwanza ya kimataifa inayotangaza kwa mtandao wa kisasa (high-definition). Kauli yake mbiu ni Setting the News Agenda.

Hii ni stesheni ya kwanza inayotangaza kwa lugha ya Kiingereza iliyo na makao yake makuu kwenye nchi iliyo Mashariki ya Kati.

Al Jazeera ina vituo vinne vikuu kote duniani, mjini London, Washington, DC, Kuala Lumpur na Doha. Ina milikiwa na serikali ya Qatar. Hii ni moja kati ya stesheni chache iliyo na ofisi zake mjini Gaza na Harare.


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu