Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Tarehe 15 november mwaka 1931 mwai kibaki Rais wa tatu wa Kenya alizaliwa

November 15, 2018

Mwai Kibaki ni rais wa tatu wa Jamhuri ya Kenya akiwa ametanguliwa na Rais wa Kwanza wa Kenya,Mzee Jomo Kenyatta, na Daniel Arap Moi. Jina lake la kubatizwa ni Emilio Stanley.

Kibaki alisoma uchumi, historia na sayansi ya siasa katika chuo kikuu cha Makerere, Kampala, Uganda. Akiwa mwanafunzi Makerere, Kibaki alikuwa ni mwenyekiti wa chama cha wanafunzi toka Kenya, Kenya Students' Association. Alipomaliza masomo yake mwaka 1955 alipewa tuzo kutokana na kufanya vyema katika mitihani. 

 

Tuzo hiyo ilimwezesha kwenda kusoma katika chuo cha London School of Economics. Alipomaliza masomo alikwenda kufundisha katika chuo kikuu cha Makerere. Baadaye aliacha kazi ya kufundisha na kuwa mtendaji mkuu wa chama cha Kenya African National Union.

Kibaki, licha ya kuwa mbunge, amewahi kuwa Naibu Waziri wa Fedha, Mwenyekiti wa Tume ya Mipango, Waziri wa Biashara na Viwanda, na Waziri wa Fedha. Moi alipoingia madarakani baada ya kifo cha Jomo Kenyatta, Kibaki aliteuliwa kuwa Makamu wa Rais.

 

Mwaka 1988 Kibaki alianza kuwa na mgongano na Rais Moi. Mwaka huo alivuliwa Umakamu wa Rais na kupelekwa Wizara ya Afya.

Mwaka 1991 Kibaki aliondoka chama cha KANU na kuanzisha chama cha Democratic Party. Katika uchaguzi wa Urais wa mwaka

1991, Kibaki alikuwa wa tatu na mwaka 1997 alikuwa wa pili.

Katika uchaguzi wa 2002 Kibaki alishinda na kutangazwa kuwa Rais wa Kenya. Alikuwa mgombea wa maungano wa vikundi vingi vya upinzani vilivyoshirikiana kwa jina la "NARC".

Kibaki ameweka historia mwezi Novemba 2005 baada ya kuwa Rais wa kwanza nchini Kenya kuondoa baraza lote la mawaziri kufuatia kura ya maoni ambayo ilikuwa inahusu katiba mpya ya Kenya. Kibaki alikuwa upande wa kundi lililokuwa likiunga mkono katiba hiyo kambi ya ndizi. Kundi lililokuwa likiipinga katiba hiyo kambi ya machungwa lilipata ushindi.

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload