Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Mtaalamu wa Astronomia,Hisabati,teolojia na Muziki kutoka nchini Ujerumani Johannes kepler alifariki tarehe 15 november 1630

November 15, 2018

Amekuwa maarufu hasa kwa sababu alitambua kanuni za mwendo wa sayari zikizunguka jua.

KAZI YAKE

 

Alianza masomo yake kwenye chuo kikuu cha Tuebingen katika fani ya theolojia akilenga kuwa mchungaji. Pamoja na Theolojia alisoma pia hisabati halafu akafuata mwito wa kuwa mwalimu wa hisabati kwenye chuo cha Kiprotestanti mjini Graz(Austria). 

 

Baadaye aliitwa Praha (leo nchini Ucheki) kama msaidizi wa Tycho Brahe aliyekuwa mwanahisabati rasmi wa KaisariRudolph II. Baadaye Kepler alipewa wajibu huu.

Sanamu ya Tycho Brahe na Johannes Kepler mjini Prague.

Kanuni za mwendo wa sayari.

  1. Kanuni ya kwanza inasema sayari inatembea njia yenye umbo la duara dufu, si duara kamili, ikizungukia jua. Kabla ya Kepler wanaastronomia waliona njia ya sayari ni duara kamili.

  2. Kanuni ya pili inasema ya kwamba sayari inaongeza mwendo ikikaribia jua, lakini inapunguza mwendo ikienda mbali na jua.

  3. Kanuni ya tatu inaeleza ya kwamba sayari iliyo karibu na jua ina mkasi mkubwa kuliko sayari ambayo ni mbali.

Sala yake

“Kwako wewe, ambaye kwa mwanga wa uasilia unachochea ndani mwetu hamu ya neema yako ili tuweze kufurahia utukufu wako, kwako natoa shukrani, Bwana wangu na Mungu wangu, kwa sababu umenifanya kuonja furaha na raha katika vile vyote ulivyoviumba, katika vile vyote vilivyo kazi ya mikono yako azizi. Tazama, ee Bwana, nimemaliza kazi hii iliyokuwa wito wangu. Ili kuifanya nimetumia ile nguvu ya akili uliyonijalia wewe. Nimewaonyesha binadamu ukuu wa kazi yako, au walau sehemu ile ya ukuu wako usio na mipaka ambayo akili yako imeweza kuelewa.

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload