Mwanamke ajifungua mtoto baada ya kupandikizwa mfuko wa uzazi India

Meenakshi Valand ni mmoja kati ya watu wachache duniani ambao wamejaaliwa kupata watoto baada ya kupandikizwa mfuko wa uzazi.

Alikuwa na furaha isiyokuwa na kifani.

"Sikuweza kujizuia kulia baada ya kusikia sauti ya mwanangu akilia. Haya ni machozi ya furaha - Nimepoteza watoto sita katika kipindi cha miaka kadhaa iliyopita," alisema Meenakshi.

Mama huyo wa miaka 28-alijifungua mwezi uliyopita nchini India baada ya kupandikizwa mfuko wa uzazi wa mamake mzazi.

Katika miaka tisa ya ndoa yake, Meenakshi alizaa watoto wawili waliofariki, alipoteza wengine wanne katika uja uzito, hatua iliyomsababisha kukatika kwa mfuko wake wa uzazi.

Hali hiyo inajulikana kama Ashermans syndrome.

Lakini hakukata tamaa. "Nilitaka kuwa na mtoto wangu mwenyewe. Sikutaka kutumia mbinu nyingine yoyote."

Kwa mujibu wa jarida la kimataifa la utafiti wa kisayansi, 15% ya watu hawana uwezo wa kuzaa na 3 kati ya 5% ya visa hivi husababishwa na matatizo ya mfuko wa uzazi.

Alimtembelea Dkt Shailesh Putambekar, mtaalamu wa upasuaji na upandikizaji wa mfuko wa uzazi katika hospitali ya Galaxy Care mjini Pune.

Wakati huo mama yake Sushila Ben alikuwa amejitolea kumpatia mfuko wake wa uzazi ili kumuezesha kupata mtoto.

Upandikizaji huo ulifanywa na kundi la wataalam 12 mwezi Mei mwaka 2017 na ulifanikiwa.


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu