Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Robert Sherwood, mwandishi Mmarekani aliyefariki tarehe 14 mwezi wa 11 mwaka 1955

November 14, 2018

 Robert Emmet Sherwood  alifariki  14 Novemba 1955) alikuwa mwandishi wa michezo ya kuigiza kutoka nchi ya Marekani. Anajulikana hasa kwa tamthili  zake zinazojishughulikia  shida za kijamii na za kisiasa.

 

Alipokea Tuzo ya Pulitzer ya Tamthiliya mara tatu: 1936, 1939 na 1941. Tena alipokea Tuzo ya Pulitzer ya Wasifu mwaka wa 1949 kwa kitabu chake Roosevelt and Hopkins.

TUZO ALIZOPOKEA ROBERT EMMET

Tuzo ya Pulitzer ya Wasifu ni aina moja ya Tuzo za Pulitzer ambazo hutolewa kila mwaka nchini Marekani. Ni miongoni mwa aina za asili zilizotolewa kuanzia 1917, na imetolewa kumheshimu mwandishi Mwarekani aliyeandika wasifu wa mtu hodari katika mwaka uliopita.

Kuanzia 1980, wagombea watatu wa mwisho walikuwa wakitangazwa, yaani mshindi mkuu pamoja na mshindi wa pili na wa tatu.

Tuzo ya Pulitzer ya Tamthiliya ni aina moja ya Tuzo za Pulitzer ambazo hutolewa kila mwaka nchini Marekani. Ni miongoni mwa aina za asili zilizotolewa kuanzia 1917, na hutolewa kumheshimu mwandishi Mwarekani aliyeandika tamthiliya hodari katika mwaka uliopita.

Kuanzia 1983, wagombea watatu wa mwisho walikuwa hutangazwa, yaani mshindi mkuu pamoja na mshindi wa pili na wa tatu.

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload