Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Mamie Eisenhower, mke wa Dwight D. Eisenhower, Rais wa Marekani kati ya mwaka 1953-1961, siku kama ya leo mwezi kama wa leo mwaka wa 1896 alizaliwa

November 14, 2018

Mamie Geneva Doud Eisenhower  alizaliwa tarehe 14 Novemba 1896  alikuwa mke wa Rais-Jenerali wa zamani wa Marekani Bw. Dwight D. Eisenhower. Alianza kuwa Mwanamke wa Kwanza wa Marekani kuanzia mwaka 1953 hadi 1961. Mamie na Eisenhower walioana mnamo mwezi Julai ya mwaka wa 1916.

 

Mamie alizaliwa mjini Boone, Iowa. Alikuwa mtoto wa mzee John Sheldon Doud. Babake na Mamie alikuwa tajiri wa kutosha, kwakuwa alikuwa anamiliki kiwanda cha kusindika nyama za kopo. Kuna kipindi, familia ya mzee Doud iliishi kidogo mjini Pueblo, Colorado.

 

kisha Familia ikahamia na kuweka makazi yake rasmi katika mji wa Denver, Colorado. Wakiwa huko, Mamie na ndugu zake wengine wa kike watatu walikulia huko wakiwa katika mazingira ya mjumba mkubwa kabisa usio na kifani. Na nyumba ilikuwa na wahudumu wengi kupita kiasi.

 

Ilipofika mnamo mwaka wa 1915 Mamie alkakutana na Bw. Dwight D. Eisenhower. Na kwa kipindi hicho Bw. Eisenhower alikuwa na cheo cha Luteni masaidizi katika Jeshi. Mwaka uliofuatia katika siku ya wapendanao duniani, wawili hao wakavishana pete ya uchumba. Na ilivyofika tar. 1 Julai ya mwaka wa 1916 wakajaaliwa kuoana.

 

 WASIFU WA DWIGHT D.EISENHOWER

Dwight David Eisenhower  alikuwa mwanajeshi na mwanasiasa kutoka nchi ya Marekani. Watu wengi walikuwa Wanamwita Ike (tamka Aik). Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia alikuwa jenerali mkuu aliyeongoza uvamizi wa Normandy tarehe 5 Juni 1944. Kuanzia mwaka wa 1953 hadi 1961 alikuwa Rais wa 34 wa Marekani. Kaimu Rais wake alikuwa Richard Nixon.

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload