Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Boutros Boutros-Ghali, mwanasiasa wa Misri, na Katibu Mkuu wa UM, wa kwanza kutoka bara la Afrika, siku kama ya leo mwezi kama wa leo lakini katika mwaka1922 alizaliwa.

November 14, 2018

Boutros Boutros-Ghali  alizaliwa 14 Novemba 1922  alikuwa mwanasiasa na mtaalamu wa sheria kutoka nchini Misri. Alikuwa katibu mkuu wa Umoja wa Kimataifa UN kati ya 1992 na 1996.

 

Alizaliwa katika familia ya Wakristo Wakopti mjini Kairo. Babu yake alikuwa waziri mkuu wa Misri. Baada ya shule alisoma sheria kwenye chuo kikuu cha Kairo akamaliza 1946 akaendelea kuchukua shahada ya udaktari huko Ufaransa.

Baada ya kufunza miaka kadhaa alipewa nafasi ya naibu waziri wa maswala ya Kigeni chini ya rais Anwar as-Sadat. Akishughulika amani kati ya Israeli na Misri alisaidia pia kutiwa huru kwa aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Nelson Mandela.

Kuanzia Januari 1992 hadi Januari 1997 alikuwa Katibu Mkuu wa UM, akiwa Mwafrika wa kwanza kwenye nafasi hii

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload