Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Tanzania: Baadhi ya wananchi wadaiwa kuharibu bustani za wazi zilizopo Dar es Salaam

November 11, 2018

Kwa jiji kubwa kama Dar es salaam ni muhimu kuwepo kwa bustani kubwa yenye ulinzi na mazingira mazuri ya kupendeza.

Baada ya purukushani za hapa na pale katikati ya jiji, baadhi hutamani kutafuta mahali pazuli ambapo wanaweza kupumzika kwa muda ili kutuliza akili wakiwa chini ya kivuli kizuri au yawezekana kuongea au kumsubiri mtu na baadae aendelee na mizunguko yake.

Hata hivyo katika jiji hili la Dar es Salaam, kuna bustani chache ambazo zinatajwa kutokuwa na ubora wala vigezo vya kuitwa bustani kwa sababu hazina matunzo.

Na moja ya changamoto ni wananchi wenyewe ambao huaribu miundombinu hasa inapokuwa mipya.

Lakini nchi jirani hali ikoje?

Kwa upande wa Kenya, wao wana bustani kubwa ya Uhuru (Uhuru Park) ambayo ilitengenezwa tangu mwaka 1969 wakati wa utawala wa Rais Jomo Kenyatta.

Uganda pia wamejitahidi sana katika kuboresha bustani ikiwemo bustani nzuri ya hifadhi za mimea ya Entebe, kuna bustani iliyopo mjini ya Equatorial ambayo wengi huitaja kuwa na kelele na bustani kubwa ya sheraton ambapo mara nyingi watoto na wanafunzi hupenda kukaa hapo na bustani nyingine nyingi.

Kwa nini bustani za Dar es Salaam zimetelekezwa?

 baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wamezungumzia juu ya matumizi ya bustani hizo za wazi kwa watu wote, Lakini kutokana na sababu mbali mbali baadhi ya wakazi wanasema ni bora kwenda katika mgahawa kuliko kukaa maeneo ya wazi ya bustani za serikali.

Ni suala la aibu kusema kwamba Dar kuna bustani za wazi looh, yaani bora kukaa bar utakunywa maji au soda yataisha maana huko kwenye bustani ndio kwanza unaskia harufu hadi ya mikojo, vibaka kila kona. Kwa kweli halmashauri imezubaa sana kwenye hili labda mseme nyie," Rashid anaiambia BBC

"Bustani zipo kama mnazi mmoja sema sijawahi kwenda alafu naijua hiyo tu na sio nzuri. Ujue kizuri chajiuza kungekuwa na bustani nzuri na joto hili ungeona watu kibao wanaenda," Jamila anaeleza.

Hata hivyo baadhi ya bustani zilizopo zinatumika kwa matukio maalumu tu na watu hawaruhusiwi kuingia bila vibali.

 Salma Mohamed Abdalla ambaye ni mfanyakazi wa manispaa katika bustani ya Botanical, yeye anasema kwamba bustani hiyo haitumiki mpaka mtu aombe kibali.

"Zamani ilikuwa wazi na wanafunzi walikuwa wanajaa hapa, lakini kama unavyoona walichomoa vibao vyote vinavyoelekeza jina na mahali ulipo toka kila mmea katika bustani hii, hapa miti yenye vibao haiwezi kuzidi nane.

Watu walifanya sana uharibifu na ndio maana pakasimamishwa kwa muda maana sasa hivi mpaka mtu akutembeze.

Hata hivyo anayehitaji kuja kukaa anaweza kuomba akaruhusiwa ingawa changamoto bado ni nyingi.

Maji hakuna na ndio maana unaona miti imesinyaa na hata vibao vinatakiwa kuwekwa tena," Salma anaeleza.

 Hata hivyo mfanyakazi huyo anasema pamoja na kuzuiwa kuingia wapo wanafunzi ambao hupanda juu ya kuta kukaa kisha wanakula na kutupa taka bustanini.

Ila anaamini kwa sasa hawawezi kufanya hivyo tena kwa sababu ya ulinzi.

 na meya wa jiji la Dar Es Salaam Isaya Mwita, anasema nikweli changamoto zipo yamkini ni kwasababu hawakuelekeza sana nguvu katika maeneo hayo kipindi cha nyuma.

"Maeneo ya wazi yapo kwa mfano mnazi mmoja au karimjee kuna bustani ya Botanical na maeneo mengine mengi yametengwa ili watu waweze kupumzika lakini kwa bahati mbaya mengine yamevamiwa na kujegwa lakini mengi yapo bado na watanzania wanaweza wakatumia," 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload