Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

TAREHE 12 NOVEMBER MWAKA 1938 RAIS WA TATU WA TANZANIA MHESHIMIWA BENJAMINI WILLIAM MKAPA ALIZALIWA

November 11, 2018

Benjamini William Mkapa (amezaliwa 12 Novemba 1938) ni Rais wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1995-2005) na Mwenyekiti wa zamani wa Chama Cha Mapinduzi, CCM .

Mkapa ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Makerere. Nafasi alizoshikilia zamani ni pamoja na kuwa afisa wa utawala huko Dodoma na Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu. Yeye pia aliongoza ujumbe wa Tanzania huko Marekani na alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje kutoka 1977 hadi 1980 na kutoka 1984 hadi 1990.

Katika mwaka wa 1995, Mkapa alichaguliwa  kuwa rais, msingi wake ulikuwa ni kampeni  ya kupambana na ufisadi na kwa kumuunga mkono kwa nguvu rais wa zamani Julius Nyerere.  Juhudi za Mkapa za kupambana na ufisadi ni pamoja na kuumba jukwaa la wazi lililoitwa Tume ya Rais juu ya Ufisadi (Tume ya Warioba) na kuongeza msaada kwa ofisi ya Kuzuia Ufisadi.

 Muhula wa pili wa miaka 5 wa Mkapa kama Rais uliisha Desemba 2005. Katika wakati wake ofisini, Mkapa alibinafsisha makampuni yanayomilikiwa na serikali na akaweka sera za soko huria. Wafuasi wake walimtetea kwa kusema  kuwa  kuvutia uwekezaji wa kigeni ungesaidia kukuza uchumi. Sera zake zilipata msaada wa Benki ya Dunia na IMF na kupelekea baadhi ya madeni ya nje ya Tanzania kufutiliwa mbali.

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload