Uchaguzi wa Marekani: Mambo 5 ambayo utawala wa Trump hauwezi kufanya bila kushauriana na Democrats


Uchaguzi wa katikati ya muhula nchini Marekani tayari ulikuwa umebashiri kwamba utaelekea upande wa chama cha Democrats na bunge la uwakilishi.

Hivyo basi kusitisha kipindi ambapo chama cha Republican na rais Trump walikuwa wakidhibiti bunge la Congress na serikali. Vitu vinne ambavyo vimebadilika katika siasa ya Marekani baada ya Democrats kuchukua udhibiti wa bunge la uwakilishi.

Katika muhula wake rais Trump amefaidika kutokana na bunge la Congress lililompendelea , bunge ambalo lilimuunga mkono kwa maneno na vitendo na kuunga mkono mipango yake ya kisiasa.

Lakini katika miezi miwili, wakati bunge jipya linalodhibitiwa na Democrats litawasili mjini Washington , kila kitu kitabadilika.

Baada ya miaka kadhaa ambapo alishinikizwa kupitishwa kwa sheria kali dhidi ya wahamiaji, kubadilishwa kwa mswada wa afya wa Obamacare mbali na kukata idadi ya mipango ya kijamii chini ya serikali ya Republicans bunge la wawakilishi sasa litaanza kuwasilisha maswala muhimu bungeni.

Utawala unaotazamwa sana

Nancy Pelosi, ambaye ndio kama rais wa bunge la uwakilishi , amewahakikisha kwamba vitu vitakavyopewa kipaumbele katika orodha ni maswala ya maadili na mabadiliko ya uchaguzi.

Sasa ni wakati wa Democrats kuona juhudi zao katika bunge le seneti, lakini wanachama wa Democrats wana eneo ambalo sasa wanaweza kulitumia kuonyesha kwamba watalithibiti bunge la Congress na pengine urais mwaka 2020.

Wakati huohuo matumaini ya rais Trump ya kupitisha sheria yatapitia kushirikiana na Democrats, swala litakalokuwa mzigo mkubwa kwa mtu ambaye amehudumu miezi kadhaa ya muhula wake akiwadharau wapinzani wake wa kisiasa kwa kutumia lugha mbaya wakati wa kampeni yake nchini humo.

Hatahivyo mtihani mkubwa wa rais huyo ni kwamba wanachama wa Democrats wanajiandaa kuchunguza utawala wake.

Kamati ya ujasusi ya bunge la uwakilishi ambayo iliongoza uchunguzi wa Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani wa mwaka 2016 -itakuwa chini ya mpinzani mkuu wa Trump Adam Schiff ambaye ameapa kupunguza matumizi ya rais Trump ugenini.

Haitachukua muda mrefu kabla ya ushuri wa rais Trump kujulikana. Wanachama wengine wa utawala wa rais Trump pia watachunguzwa.

Mambo 5 ambayo rais Trump hatoweza kuidhinisha utekelezwaji wake.

Kushindwa kwa utawala wa rais Trump kudhibiti bunge la uwakilishi kutapunguza uwezo wa rais Trump kufuatilia ajenda yake ya kisiasa , kwa kuwa ifikapo mwezi Januari atalazimika kujadiliana na uongozi wa chama cha Democrat katika mji mkuu ili kuidhinishwa.

Baadhi ya mipango ya Trump ambayo haitadhinishwa ni pamoja na:

1.Ujenzi wa ukuta na Mexico: Ukuta huo ambao rais Trump ameahidi kujenga katika kampeni za mwaka 2016 utagharimu mammilioni ya madola ambayo lazimia yaidhinishwe na bunge la Congress. Ijapokuwa haijafutiliwa mbali kwamba kupitia majadiliano chama cha Republican kinaweza kupata ufadhili kutoka idara tofauti.

2.Kubadilisha mswada wa afya wa Obamacare: Chama cha Republican chenyewe haikukubaliana kubadilisha mswada wa afya wa Obamacare.Na sasa Democrats wakiwa na uwezo wa kudhibiti bunge la uwakilishi, uwezo wa kuondoa sheria hiyo haupo tena kwasababu kwa sababu waliahidi kuutetea mswada huo wakati wa kampeni zake

.

3.Mabadiliko ya uhamiaji: Kuondolewa kwa lotari ya Visa, kupunguza uwezekano wa familia za wahamiaji kukutana na kuanzisha mfumo wa uhamiaji utakaopendelea serikali ni miongoini mwa mapendekezo ambayo serikali ya rais Trump ilijaribu bila mafanikio katika kipindi cha miaka miwili iliopita. Na sasa uwezekano wa mipango hiyo kuendelea inazidi kudidimia.

4.Kuondoa uraia wa kuzaliwa: Mwisho wa mwezi uliopita , rais Trump alitangaza lengo lake kumaliza uraia wa kuzaliwa nchini Marekani kupitia amri ya rais. Pendekezo hilo lilipingwa kwa sababu ni sheria iliopo katika katiba ambayo ina uwezo mkubwa zaidi ya maamuzi ya rais. Mbadala wa kuliangazia swala hilo ni kufanya marekebisho ya katiba , ambapo ni muhimu kupata uungwaji mkono ya thulkuthi mbili kwa bunge la Congress pamoja na lile la uwakilishi lakini hakuna ishara kwamba unaweza kupata uungwaji mkono.

5.Kupunguza tozo: Mwisho wa 2017 , chama cha Republican chenye wabunge wengi wa Congress na Ikulku ya White house walijadiliana na kukubaliana kuweka sheria ya kumpunguza tozo miongoni mwa raia wake,kwa muda na kampuni kudumu. sheria hiyo ilikosolewa sana na wananchama wa Democrats ambao walisema utawafaidisha watu matajiri zaidi na ya raia wengine.

na kampuni kudumu. sheria hiyo ilikosolewa sana na wananchama wa Democrats ambao walisema utawafaidisha watu matajiri zaidi na ya raia wengine


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu