NCHI YA ANGOLA YAPATA UHURU TAREHE 11 NOVEMBER 1975

November 11, 2018

tarehe  11 mwezi wa november mwaka  wa 1975 nchi ya angola ilijipatia uhuru baada ya kutawaliwa kwa  muda mrefu  na taifa  la wareno kwa zaidi ya  miaka 300.

Angola ni nchi kubwa iliyopo upande wa kusini wa bara la Afrika ikipakana na Namibia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na Zambia. Upande wa magharibi kuna pwani ndefu ya Bahari ya Atlantiki. Mkoa wa Kabinda umetenganika na sehemu nyingine za nchi na unapakana na Jamhuri ya Kongo pia.

Angola ni nchi tajiri kwa mafuta na madini: almasi ndiyo muhimu zaidi. Lakini nchi ni maskini kutokana na vita vya miaka 29; kwanza vita vya kupigania uhuru dhidi ya Ureno iliyofuatwa na vita ya wenyewe kwa wenyewe hadi mwaka 2002.

Nchi yenyewe hasa ni ya kidemokrasia na inajulikana kama Jamhuri ya Angola (kwa Kireno: República de Angola, kwa matamshi ya IPA: /ʁɛ.'pu.βli.kɐ dɨ ɐ̃.'ɣɔ.lɐ/; kwa lugha za wenyeji: Repubilika ya Ngola)

 

Jina Angola linatokana na neno la lugha ya Kibantu "N’gola", ambalo lilikuwa jina la kiongozi wa ufalme wa Kwimbundo karne ya 16, ambapo Wareno walianza ukoloni katika eneo hili.

 Wakazi wa kwanza huaminiwa kuwa wawindaji wa jamii ya Wasani.

Katika karne za kwanza BK kutoka kaskazini walifika wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi.

Kuanzia karne ya 14, falme mbalimbali zilienea sehemu za Angola, kwa mfano Dola la Kongo, Dola la Lunda na Dola la Kasanje.

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon