Michelle Obama afichua jinsi alivyoshika uja uzito wa watoto wake 2

November 10, 2018

Aliyekuwa mke wa rais wa Marekani Michelle Obama ametoa kumbukumbu ambapo amefichua matatizo aliyopitia katika ndoa yake na uja uzito wa watoto wake wawili.

Katika kitabu hicho, Becoming, Bi Obama amefichua kwamba alitokwa na ujauzito na akalazimika kutumia mbinu ya IVF ambapo mayai ya wapendanao huchanganywa nje na baadaye kuwekwa katika kizazi cha mwanamke kupitia sindano.

 

Bi Obama aliambia kituo cha ABC Good morning America kwamba alihisi 'amepotea na mpweke' baada ya kupoteza uja uzito miaka 20 iliopita.

 

Pia alimkosoa rais Donald Trump kwa kuweka usalama wa familia yake hatarini . Bi Obama na mumewe, aliyekuwa rais wa Marekani Barack Obama walilazimika kufanyiwa vikao vya ushauri , na pia alifichua kwamba kwa mara ya kwanza katika kitabu chake chenye kurasa 426 kitakachotolewa siku ya Jumanne.

Kufuatia kuchapishwa kwa kitabu hicho Bi Obama atatembelea miji 10 ikiwemo London.

 

Alipokuwa mjamzito

 

Bi Obama , wakili wa zamani na msimamizi wa hospitali aliambia ABC kwamba baada ya kupoteza uja uzito, nilihisi kwamba nimefeli kwasababu sikujua takwimu za kumwagika kwa uja uzito.

''Tunajitenga tukiwa na uchungu'', alisema  na kuongezea kuwa ''ni muhimu kuzungumza na akina mama wachanga kuhusu ukweli kwamba uja uzito unaweza kukutoka'

 Alisema kwamba alipokuwa na umri wa miaka 34, aligundua muda wa kibaiolojia upo na kwamba uzalishaji wa mayai ni mdogo swala lililomshinikiza kutafuta mbinu ya IVF.

 

'Nadhani ni kitu kibaya zaidi tunachofanyiana sisi kama wanawake kwa kutoambiana ukweli kuhusu miili yetu na vile inavyofanya kazi'', bi Obama alimwambia mwandishi wa ABC Robin Roberts katika kipindi cha Good Morning America.

 Kuhusu ndoa yake

 

Bi Obama alifichua kwamba ndoa yao ilikumbwa na misukosuko mingi, hususan baada ya mumewe kujiunga na bunge la jimbo hilo , na hivyo basi kumwacha nyumbani ambapo alilazimika kutumia sindano za IVF mwenyewe.

 

''Ushauri katika ndoa yetu kwetu sisi ulikuwa mojawapo ya njia ambapo tulijua kushughulikia tofauti zetu'', aliambia ABC.

 

'Najua wanandoa wengi wachanga ambao wanakabiliwa na changamoto na nadhani kuna makosa wanayofanya, Na nataka wajue kwamba bi Michelle na Barrack Obama ambao wamekuwa na ndoa nzuri na ambao wanapendana sana, pia huketi chini na kuimarisha ndoa yao. na tunapata usaidizi wa ndoa yetu tunapohitaji''.

 

Kuhusu Trump

 Katika kitabu hicho cha in Becoming, Bi Obama anasema hatomsamehe tena rais Trump kwa kusema kuwa mumewe sio mzaliwa wa Marekani wakati wa kampeni yake ya urais kulingana na habari zilizochapishwa katika vituo vya habari.

Swala lote la alikozaliwa Obama lilikuwa la kukera. Je ingekuwaje iwapo mtu ambaye hana akili timamu angechukua bunduki na kuelekea Washington ? Je iwapo mtu huyo angekwenda kuwatafuta wana wetu?.

''Trump na tabia zake alikuwa akiweka familia yangu hatarini''.

Anasema kuwa alishangazwa sana na ushindi wa rais Trump

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

'.

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon