Mexico yafungua vituo miji 50 nchini Marekani kutetea raia wake


Mexico imefungua vituo vya kutoa msaada wa kisheria katika balozi zake katika miji 50 ya Marekani, ili kulinda raia wake kutokana na utekelezaji mkali wa sheria za uhamiaji nchini humo.

Wakati wa ziara ya maafisa wakuu wa Marekani nchini Mexico mwezi uliyopita, utawala wa nchi hiyo ulielezea wasiwasi wake juu ya sera ya Trump ya uhamiaji dhidi ya raia wake.

  • Rais wa Mexico afuta ziara yake Marekani

  • Wahamiaji wasio na vibali wakamatwa Marekani

  • Bidhaa za Mexico kutozwa kodi Marekani

Inakadiriwa kuwa takriban raia milioni sita wa Mexico wanaishi nchini Marekani kinyume cha sheria.

Vituo hivyo vipya vitatoa msaada wa sheria Kwa raia wa Mexico ambao wanahisi kuwa haki zao ziko hatarini nchini Marekani.

Uhusiano kati ya Mexico na Marekani umekuwa mbaya zaidi tangu miango kadha iliyopita.

Wiki moja baada ya kuapishwa mwezi Januari , Rais Donald Trump alisema kuwa atajenga ukuta kati ya mpaka wa Mexico na Marekani.

  • Trump tutajenga katika mpaka wa mexico

  • Marekani kujenga ukuta mara moja

Alisisitiza kuwa Mexico italipia gharama ya ujenzi wa ukuta huo.

Matamshi hayo yalisababisha rais wa Mexico Enrique Pena Nieto, kufuta safari yake nchini Marekani tarehe 31

mwezi Januari. na kutangaza ufadhili zaidi kulinda haki za za raia wa Mexico walio nchini Marekani.


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu