PICHA:Shilole apata deal ya kusoma British Council baada kushindwa kutamka ‘Subscribe’

Baada ya kuchekwa sana kwa kutojua kiingereza, msanii wa Bongo Flava Shilole aingia kwenye mkataba na shirika la uingereza British Council Tanzania ili kujifunza lugha hiyo.

 

Mbali ya muziki, msaani huyo anajulikana sana kwa kuwa na hamasa ya kuongea kiingereza bila kujali makosa ambayo anayafanya.

 

Wiki iliyopita video ya mtandao wa Bongo5  ilitrend ikimuonyesma muimbaji huyo akishindwa kumtamka neno “Subscribe”.

 

Shirika la Uingereza British Council Tanzania, limefurahi Shilole ameamua kutaka kujiendeleza katika lugha ya kiingereza ambayo itamsaidia katika kazi yake kama msanii.

 

Angela Hennelly, Country Director, amesema kuwa ni fursa nzuri kwa Shilole kujua lugha ya Kiingereza na amempongeza kwa hatua hiyo aliyoichukua

 

Ameendelea kusema kuwa hii itamfungulia milango mingi ya fursa kulingana na jinsi uchumi wa dunia unavyokua na changamoto wanazozipata haswa wasanii.

 

Angela ameendelea kusema kuwa anategemea hii fursa itawapa moyo vijana kufikiria pia kujiendeleza katika lugha ili waweze kufanya mawasiliano kwa urahisi katika shughuli zao za kila siku haswa kwa upande wa ajira..

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon