SABABU YA KUNYONGA WATOTO MAPACHA SIKU YA 3 BAADA YA KUZALIWA


Leo May 23, 2018 Katika kijiji cha Kaida, Gwagwalada katika jimbo la Abuja nchini Nigeria, wanawanyonga watoto mapacha siku ya tatu tu baada ya kuzaliwa kwa kile wanachoamini kuwa watoto mapacha ni mashetani hivyo inabidi wauawe kwa kunyongwa.


Taarifa hizo zimekuja baada ya asasi inayojulikana kama Peach Aid Medical Iniatiative medical Doctors kudhuru katika kijiji hicho na ndipo mwanamke mmoja katika hali ya kushangaza aliifuata timu ya asasi hiyo na kuwaomba kuwachukua mapacha wake ambao ndio kwanza walikuwa na siku mbili tu tangu wazaliwe.


Mmoja wa wana asasi hiyo alipomuuliza kwa nini wawachukue watoto hao mapacha, mwanamke huyo alimwambia kuwa akibaki nao watauawa siku za usoni maana katika kijiji hicho mapacha wanachukuliwa kama mashetani na huuawa kwa kunyongwa siku ya tatu baada ya kuzaliwa.


Aidha mwanamke huyo aliiambia timu ya asasi hiyo kuwa mapacha hao walikuwa ni mimba yake ya nne akiwa ana bahatika kupata mapacha katika mimba zake zote hizo nne.


Hata hivyo timu nzima ya asasi hiyo ilifanikiwa kuokoa maisha ya mapacha hao.


MZunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu