GARI YA KUBEBA WAGONJWA (AMBULANCE) YAPATA AJALI HUKU IKIWA NA WAGONJWA MAHUTUTI.


Ni usiku wa tarehe 22/05/2018 majira ya saa 4 usiku maeneo ya sinza mori imetokea ajari ya gari aina ya HARRIER kugongana na AMBULANCE iliyokua imebeba wagonjwa ambao ni akina mama wajawazito waliokua wakiwaishwa Hospitali kwa ajili ya kupata matibabu.

Kwa bahati nzuri hakuna mtu ata mmoja ambae ameumia au kupatwa na jeraha lolote kutokana na ajali hiyo ila pia tumeweza kuona baadhi ya Mapolisi na Madaktari waliokua vituo vya karibu waliweza kufika katika eneo hilo la tukio na kuwasaidia kuwatoa kwenye AMBULANCE ya kwanzana kuingia kwenye AMBULANCE ya pili na kuwaishwa Hospitalini ili wakapate matibabu.


Pia waandishi wetu wa habari kutoka GenerationWorks (mzunguko online) walifanikiwa kufika kwenye eneo la tukio na kuweza kuchukua baadhi ya maelezo kutoka kwa wakazi na wafanya biashara mbalimbali waliokua karibu na eneo hilo na pia walioshuhudia tukio hilo.

ENDELEA KUWA NASI KWA HABARI NA MATUKIO MBALIMBALI YA NDANI NA NJE YA NCHI

Mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu