KIM JONG-UN AONYWAMakamu wa Rais wa Marekani Mike Pence amemuonya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un kuwa asimchezee Rais Donald Trump ikiwa watakutana mwezi ujao.

"Yatakuwa ni makosa makubwa kwa Kim Jong-un kufikiri kuwa atamchezea Donald trump," Bw Pence alisema wakati akihojiwa na kituo cha Fox News.

Bw Pence pia alisema kuwa Bw Trump anaweza kuondoka kwenye mkutano huo wa Juni 12.


Korea Kaskazini imetisha kujitoa mkutano huo baada ya matamshi ya mshauri wa masuala ya ya ulinzi nchini Marekani John Bolton.

Korea Kaskazini ilijibu vikali walati Bolton alisema kuwa itafuata mfumo wa Libya katika kuondoa zana za nyuklia.


Kingozi wa zamani wa Libya Muammar Gaddafi alikubaliana na mataifa ya Magharibi mwaka 2003 kuharibu mpango wake ili apate kuondolewa vikwazo. Miaka minane baadaye aliuawa na waasi walioungwa mkono na nchi za Magharibi.

Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in ana mpango wa kukutana na Bw Trump mjini Washingiton leo Jumanne kuzungumzia mipango ya mkutano huo.


Bw Pence alisema hakuna shaka kuwa Bw Trump ana nia ya kuondoka kwenye mkutano huo ambao unapangwa kufanyiwa nchini Singapore.

​"Sifikiri kuwa Rais Trump anafikiri kuhusu sifa, anachofikiri ni kuhusu amani," Pence alisema.

Gazeti la New York Times liliripoti Jumapili kuwa Trump alikuwa ameulizwa na wasaidizi na washauri wake ikiwa anaweza kuendelea na mkutano huo.


mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu