EDEN HAZARD NA JOSE MOURINHO WANA UGOMVI?

 

 Ni kitu cha kawaida au mara nyingi imezoeleka kuonekana kama wachezaji waliocheza pamoja au kocha na mchezaji ambao wamewahi kufanya kazi pamoja wakikutana mara nyingi wanaonekana kusalimiana kwa furaha.

Hii imekuwa tofauti kidogo kwa kocha wa Man United Jose Mourinho na staa wa Chelsea Eden Hazard pale walipokutana katika mchezo wa fainali ya Kombe la FA uliyochezwa Wembley.

Zimenaswa video za Jose Mourinho na Hazard kabla ya Chelsea na Man United kuingia uwanjani wakiwa katika tannel hawajasalimiana wala kuongea kitu ambacho kimezua maswali na watu kuanza kuamini kuwa Mourinho na Hazard wanatatizo.

Mchezo huo ulimalizika kwa Chelsea kupata ushindi wa goli 1-0 lililofungwa na Eden Hazard lakini wakati wa kuingia uwanjani wakiwa katika tunnel Mourinho alionesha kusalimiana na Cesc Fabregas licha ya kuwa walikuwa karibu na Hazard kila mmoja alionesha kumpotezea mwenzake.

 

Mzunguko.com #OngezaMaarifaBadilishaDunia

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon