Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

CHANJO YA EBOLA KUTOLEWA CONGO

May 21, 2018

 

 

 

 

Shirika la afya Duniani (WHO) na Serikali ya Jamhuri ya Kidemkrasi ya Congo leo wameanzisha mpango wa kutoa chanjo ya majaribio dhidi ya ugonjwa wa Ebola ili kudhibiti kusambaa zaidi kwa virusi vya ugonjwa huo.

WHO linasema limewatambua zaidi ya watu 500 ambao huenda wamkaribiana na waathiriwa wa ugonjwa wa Ebola nchini Congo.

 

Huenda watakuwa miongoni mwa watu wa kwanza leo watakaopewa chanjo hiyo ya majiribio.

Awamu ya kwanza ya chanjo hiyo ya majaribio iliwasili nchini Congo siku ya Jumatano.

Kumekuwa na milipuko mitatu ya Ebola nchini DRC tangu janga la mwaka 2014-2016 katika Afrika ya magharibi.

 

Uchunguzi uliofanyiwa chanjo ya ugonjwa wa Ebola mwaka jana umebaini kuwa inaweza kumkinga mtu kutokana na virusi vya ugonjwa huo kwa takriban mwaka mmoja.

Utafiti huo uliochapiswa katika jarida la New England Journal of Medicine, ulifanyiwa nchini Liberia na kuwashirikisha wagonjwa 1,500.

Wale waliopewa chanjo hiyo walifanikiwa kupata kinga yenye nguvu kwa karibu mwaka mmoja.

 

Majaribio hayo yanaonyesha kuwa chanjo hizo zote zinaweza kutumiwa kuokoa maisha wakati wa majanga ya ugonjwa wa Ebola siku za usoni.

Ugonjwa wa Ebola uliwaua zaidi ya watu 11,000 nchini Liberia, Sierra Leone na Guinea, wakati wa mlipuko wa ugonjwa huo mwaka  2014-2015.

 

Mzunguko.com

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload