Chelsea watwaa ubingwa wa kombe la FA, Bayern Munich wafanyiwa umafia fainali ya DFB Pokal

May 20, 2018

Klabu ya Chelsea jana usiku imetwaa kombe la FA kwa kuiadhibu Manchester United goli 1-0 kwenye mchezo uliochezwa kunako dimba la Wembley.
 

 

Goli pekee la Chelsea lilifungwa na Eden Hazard kunako dakika ya 22 kwa njia ya mkwaju wa penati. 


Wakati klabu ya Chelsea ikitwaa ubingwa huo, Klabu ya Bayern Munich usiku huo huo kwenye fainali za kombe la BFB Pokal nchini Ujerumani wameambulia kipigo kitakatifu cha goli 3-1 dhidi ya Eintracht Frankfurt. 

 

 

 

Frankfurt ndio walikuwa wa kwanza kutikisa nyavu za Bayern Munich kunako dakika 11 kupitia kwa Ante Rebic kabla ya Robert Lewandowski kusawazisha goli hilo kunako dakika ya 53.

Hata hivyo, Bayern hali ilizidi kuwa ngumu uwanjani baada ya Frankfurt kuongeza goli la pili kupitia kwa Ante kunako dakika 80 huku goli la tatu likifungwa na Mijat Gacinovic.

Klabu ya Frankfurt imetwaa ubingwa huo kwa mara ya kwanza kwa miaka 30 iliyopita yaani tangu mwaka 1988 walivyofanya hivyo. 

 

Mzunguko.com

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon