PICHA ZA ATHLETICO MADRID WAKISHEREKEA UBINGWA KATIKA VIUNGA VYA JIJI LA MADRID


Mabingwa wapya wa kombe la Europa Athletico madrid wametua katika jiji la Madrid wakiwa na furaha kubwa baada ya kutwaa kombe hilo siku ya jumatano tarehe 16 mei mwaka huu.Mabingwa walilakiwa na wananchi na mashabiki wa timu hiyo waliojikusanya barabarani kusherekea ubingwa pamoja na timu yao,Ikumbukwe kuwa katika fainali hiyo walikutana na timu ya Ufaransa (Marseille)na kuichabanga kwa magoli 2 kwa bila,Athletico madrid wanakuwa timu ya kwanza kupeleka ubingwa mkubwa kama huo jijini hapo huku wakiisubiri Real madrid kama wanaweza kupeleka ubingwa wa UEFA champions wiki ijayo ambapo watakutana na Liverpool ya nchini Uingereza.


Wachezaji walionekana wakiwa na furaha sana huku wakitoa maneno ya kuwashukuru mashabiki kwa kuwaunga mkono tangu walioanza mashindano mpaka hivi sasa,Ath Madrid wanshika nafasi ya pili katika ligi ya nyumbani huku bingwa akiwa tayari ashajulikana ambaye ni barcelona.

MZUNGUKO.COM


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu