ELTON JOHN KUTUMBUIZA HARUSI YA PRINCE HARRY,ULINZI WAIMARISHWA

Mwanamuziki nguli na nyota Uingereza, Sir Elton John imeripotiwa kuwa amethibitisha kutumbuiza kwenye harusi ya Prince Harry na Meghan Markle inayotarajiwa kufanyika leo May 19, 2018.

Kwa mujibu wa TMZ, mwanamuziki huyo mwenye miaka 71 anatarajiwa kutumbuiza wageni katika kasri la Windsor ingawa bado haijawa wazi iwapo atatumbuiza pia katika sherehe za kanisani au kwenye hafla iliyoandaliwa baada ya harusi.


Taarifa hiyo imekuja ikiwa imepita miaka takribani 21 tangu atumbuize wimbo wake wa Candle in the Wind kwenye mazishi ya mama mzazi wa Bwana harusi Harry, Princess Diana mwaka 1997 baada ya kufariki duniani kufuatia ajali ya gari.

Katika harusi hiyo maandalizi muhimu yamekamilika, huku ulinzi ukiimarishwa na wageni takribani 2500 wanatarajiwa kushiriki shughuli hiyo wakiwemo marafiki wa karibu wa Meghan kutoka nchini Marekani na Canada ambao tayari wameshawasili jijini London pamoja na askari na marafiki wa karibu wa Harry.

Mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu