JACK WILSHERE ALALAMIKA KUTOITWA TIMU YA TAIFA YA UINGEREZA KWENDA URUSI


Wakati mataifa mbalimbalu duniani yanayoshiriki fainali za michuano ya Kombe la Dunia kwa mwaka 2018 yanaendelea kutangaza vikosi vyao vitakavyoshiriki michuano hiyo huku wengine wakitaja vikosi vya awali, England imetaja tayari vikosi vya wachezaji 23 huku kocha wao Gareth Southgate akithibitisha kabisa Jack Wilshere na Joe Hart hawatokuwa sehemu ya kikosi chake.


Ikiwa imepita siku moja toka kikosi cha timu ya taifa ya England kitangazwe huku wakikosekana wachezaji kadhaa ikiwemo Jack Wilshere wa Arsenal, staa huyo ameshindwa kuvumilia kukaa kimya na hatimae ameamua kufunguka kutokana na kusikitishwa na maamuzi ya kocha huyo.


Kupitia twitter aacount yake Jack ameandika “Kama ningepewa nafasi ningeweza kuwa na mchango mkubwa hata hivyo nalazimika kuheshimu maamuzi ya makocha na ningependa kukitakia kikosi chote kila la kheri katika mashindano hayo, siku zote nitakuwa shabiki wa England na nitawasapoti, nimehuzunika kukosekana kuitwa katika kikosi cha England kwa ajili ya Kombe la Dunia”

mzunguko.com
Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu