Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

UWEPO WA MESSI ULIVYOLETA MSISIMKO AFRIKA YA KUSINI

May 18, 2018

 

 

 

 

Uwepo wa mwanasoka Lionel Messi nchini Afrika Kusini kumezua hisia kubwa miongoni mwa mashabiki wa soka kwa siku tatu mfululizo baada ya mchezaji huyo nyota kutoka Argentina kufanya ziara nchini humo akiwa na timu yake ya Barcelona.Mshindi wa mara tano wa tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka katika mechi waliyocheza timu ya Barca iliinyuka timu ya Mamelodi Sundowns 3-1.

Kundi la wanamichezo hao wa Barcelona lililopata nyota limefika Afrika Kusini ambako wanatarajiwa kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya mabingwa wa ligi ya Rainbow, Mamelodi Sundowns,

 

Mchezo wa kirafiki wa jumatano,baina ya Barcelona dhidi ya timu ya Sundowns baada ya mechi ya mwaka 2007, iliyopigwa katika uwanja wa Soccer City mjini Johannesburg kama mchezo wa kushereheke miaka mia moja ya Nelson Mandela raisi wa kwanza mweusi nchini humo, Mandela aliwakilisha mapambano ya uhuru na usawa , na alifanya jukumu kubwa katika kuunganisha jamii iliyogawanyika katika misingi ya ukabila hiyo ni aina ya roho ambayo Barcelona daima inatambuwa.

 

Messi hata hivyo alipata homa ya mafua na dakika ishirini kabla ya mpira kwisha aliingia uwanjani, alisababisha mashabiki kuweweseka kwa furaha na kupayuka kwa sauti pindi walipomwona nyota huyo akipasha.

 

 

 

Messi hakuonekana haraka uwanjani mpaka pale mpira ulipoanza, alionekana ni mwenye kujihifadhi zaidi kutokana na hali ya hewa ya baridi iliyotawala na kwenda kuchukua nafasi kwenye benchi la wachezaji, ingawa wapiga picha za televisheni walionesha mashabiki wa kike wakitokwa na machozi kwa kumuona Messi nchini mwao, ndani ya uwanja mmoja na kumshuhudia nyota anayecheza kwenye ligi ya Hispania amejitokeza na kupiga jaramba.

 

Ingawa alionekana kwa muda mfupi Messi, baadhi ya mashabiki 75,000 walipata picha ya ubora wa nyota huyo aliye bora duniani, na baadaye wachezaji wa timu ya Sundowns walipokuwa wakimgombea kwa kupiga picha binafsi .

Mechi hiyo ya kirafiki iliandaliwa kwa haraka, ambayo Barcelona ililipwa kiasi cha yuro milioni tatu kutoka kwa mmiliki na bilionea wa Sundowns Patrice Motsepe, aliyekuwa akisherehekea kumbikizi ya miaka 100 tangu kuzaliwa kwa Mandela.

 

mzunguko.com

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload