Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

TRUMP NA KIM WAANZA MALUMBANO TENA

May 18, 2018

 

 

 

Rais wa Marekani Donald Trump ametoa matamshi yanayokinzana na ya mshauri wake wa masuala ya usalama wa taifa, akisema mfumo wa Libya wa kumaliza zana za nyuklia hauwezi kutumiwa nchini Korea Kaskazini.

Pendekezo la John Bolton liliighadhabisha na kuitia wasiwasi Korea Kaskazini ambayo ilitisha kujitoa kwa mkutano na Trump wa mwezi ujao.

Mwaka 2003 kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi alikubali kuachana na mpango wake wa silaha za nyuklia ili apate kuondolewa vikwazo na mataifa ya Magharibi.

 

 

Huku Bolton akitazama, Rais Trump alisema: "Mfumo wa Libya si mfumo tuko nao kabisa wakati tunafikiri kuhusu Korea Kaskazini."

Makubaliano ambayo Bw Trump alikuwa akizungumzia na Kim Jong-un ni kitu ambacho Kim atakuwepo, atakuwa nchini mwake, ataiongoza nchi yake na nchi yake itakuwa tajiri sana.

 

Tangazo la Korea Kaskazini kuwa huenda ikajitoa kwa mkutano na Marekani lilinyooshea kidole mshauri wa usalama wa taifa wa Marekani John Bolton.

"Hatufichi hisia zetu dhidi yake," ilisema tarifa ya Jumatano, ambayo iliandikwa na naibu waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Korea Kaskazini Kim Kye-gwan.

Korea Kaskazini ilikuwa ikimaanisha mahojiano ya Bolton aliyoyafanya akiufananisha na hali iliyotokea Libya katika kumaliza zana za nyuklia

 

Mwaka 2003 Kanali Muammar Gaddafi alikubali kuachana na mpango wake wa kustawisjha silaha za maangamizi makubwa kwenye tangazo lililoishangaza dunia.

Vikwazo vingi vya Marekani dhidi ya Libya viliondolewa ndani ya miezi michache na uhusiano wa kidiplomasia ukarejeshwa.

Lakini mwaka 2011 Gaddhafi alipinduliwa na waasi wakiungwa mkono na majeshi ya mataifa ya shirika la kujihami la nchi za Magharibi Nato.

Baadaye alikamatwa na kuuawa na vikosi vya waasi.

 

mzunguko.com

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload