Tufuate kupitia:
 • YouTube Social Icon
 • Twitter Social Icon
 • Black Instagram Icon
 • Facebook Social Icon

BURUNDI YAPIGA KURA KUMUONGEZEA RAISI MUDA WA KUSALIA MADARAKANI

May 17, 2018

 

 

 

 

Burundi inafanya kura ya maamuzi hapo inayopania kuongeza muhula wa rais kutoka miaka tano hadi saba.

Marekebisho hayo ya katiba yakiidhinishwa na wananchi huenda rais Pierre Nkurunziza akaongoza taifa hilo hadi mwaka wa 2034.

Lakini kampeni hizo zimechafuliwa na tishio za upinzani kususia kura hiyo ya maamuzi huo na pia madai kwamba serikali imekuwa ikiwatisha wafuasi wa upinzani.

 

Umoja wa mataifa unahofia huenda ghasia zikazuka baada ya mauaji ya watu 26 hivi majuzi.

Wiki jana, washambuliaji ambao serikali imewataja kuwa magaidi, walivamia jiji la Chibitoke, wakafanya mauaji ya kiholela na kuaminika kutorokea taifa jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Image captionRais Nkurunziza amepiga kura yake kituoni ECOFO Buye, tarafani Mwumba, Mkoa wa Ngozi

 

Serikali inaamini kuwa walikuwa wanajaribu kukomesha kura ya maoni kwa kutia watu woga na kuvuruga amani.

Hali hii ikiendelea huenda warundi wengine wasipige kura.

Ni kura tata yenye matokeo makubwa.

Image captionMwandishi wetu anasema wapiga kura wamejitokeza kwa wingi vituoni

 

Rais Pierre Nkurunziza amekuwa akipiga kampeni nchini humo, akiwarai wananchi kuwa katiba hii mpya ni ya manufaa kwao.

Lakini wanaopinga wanamwona rais kama aliye na tamaa ya kukwamilia uongozi.

 

Warundi wanaulizwa kuchagua pendekezo la kuongeza muda wa kuwa rais kutoka awamu ya miaka tano hadi saba, ambayo itamwezesha Nkurunziza, ambaye amekuwa uongozini tangu mwaka wa 2005, kuendelea usukani kwa miaka mingine kumi na nne muda wake utakapokamilika mnamo mwaka wa 2020.

 

mzunguko.com

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

  Share on Facebook
  Share on Twitter
  Please reload