MAANDAMANO YAFANYIKA GAZA BAADA YA WAPALESTINA 59 KUUAWA KWA MAKOMBORA YA ISRAELMaandamano makubwa yamefanyika tena leo hii,(15.05.2018) ikiwa ni baada ya jeshi la Israel kuwauwa Wapelestia 59 wakati wa vurugu na maandamano katika eneo la mpakani la Ukanda wa Gaza.Ndugu wa Mahmoud Abu Teima ambae aliuwawa kwa makombora ya Israel

Mauwaji hayo ambayo yameingia katika rekodi ya kuwa mabaya zaidi kutokea kwa siku katika mgogoro huo kwa miaka kadhaa, yanatokana na hatua ya waandamanaji kupinga hatua ya Marekani kufungua ubalozi wake mjini Jerusalem.


Wapalestina leo hii wanaadhimisha siku wanayoiita Nakba, yaani Janga, siku ambayo zaidi ya watu 700,000 ambao walikimbia au kufukuzwa katika vita ya mwaka 1948 vilivyozingirwa na uanzishwaji wa taifa la Israel. Kumbukumbu hiyo inakuja siku moja baada ya Marekani kuuhamisha ubalozi wake kutoka Tel Aviv, kwenda katika jiji lenye mgogoro la Jerusalem , hatua mabayo imewakasirishwa Wapalestina na kulaaniwa na jumuiya ya kimataifa.

Mbinu za mauwaji ya GazaKufuatia hali hiyo kwa upande wao Iran imesema maafisa wa Israel wanapaswa kushitakiwa kama waalifu wa kivita kutoka na mauwaji ya waandamanaji. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Bahram Ghasemi ameitaka jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua za haraka dhidi ya Israel. Aidha nae Spika wa Bunge la Iran Ali Larijani ameuzungumzia uamuzi wa Israel kuuhamisha ubalozi wake Jerusalem kuwa ni sehemu ya kuzidharau taasisi za kimataifa, ikiwa sawa kabisa na kujiondoa katika mkataba wa mabadiliko ya tabia nchi wa Paris na makubalianbo ya nyuklia ya Iran.mzunguko.com
Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu