JPM KUIKABITHI SIMBA KOMBE SIKU YA JUMAMOSI

May 15, 2018

 

 

 

Uongozi wa shirikisho la soka Tanzania (TFF) kupitia Rais wake Wallace Karia, umetuma maombi kwa Waziri mwenye dhamana ya michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amuombe Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akabidhi kombe la VPL kwa Simba SC ambao ndiyo mabingwa wa msimu huu 2017/18. 


Simba itakabidhiwa kombe hilo siku ya Jumamosi Mei 19, 2018 baada ya mchezo wao wa mwisho wa ligi kwenye uwanja wa nyumbani (uwanja wa taifa) dhidi ya Kagera Sugar. 


Siku hiyohiyo pia Rais Magufuli atakabidhiwa kombe la CECAFA U17 Championship na timu ya vijana ya U17 'Serengeti Boys' baada ya timu hiyo  kushinda kombe hilo Aprili 29, 2018 nchini Burundi. 


"Tumeandika barua kwa Waziri Mwakyembe amuombe ili Rais Magufuli akabidhiwe kombe la CECAFA U17 baada ya timu yetu kufanikiwa kushinda kombe hilo huko Burundi. Waziri amesema atajitahidi kwa kila njia ili Rais akubali." 
"Pia kwa sababu siku hiyo Simba itakuwa inacheza mechi yake ya mwisho ya ligi kwenye uwanja wa nyumbani, tunafanya utaratibu Rais Magufuli awakabidhi kombe lao la ubingwa wa ligi kuu."

 

Mzunguko.com

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon