CANTONA KURUDI MANCHESTER (old trafford)Mchezaji wa zamani wa Manchester United na Ufaransa Eric Cantona anatarajiwa kurudi katika uwanja wa OLd Trafford mnamo mwezi Juni.

Atacheza katika uwanja wa Manchester United katika mechi ya hisani ya shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watoto Unicef.


Raia huyo mwenye umri wa miaka 51 anasema kuwa: Hakuna mahali pazuri kama nyumbani .

​Kujua kwamba nitarudi katia uwanja wa OLd Trafford ni hisia maalum.Atajiunga na idadi kubwa ya watu maarufu duniani akiwemo Usain Bolt na mO Farah , Olly Murs na Gordon Ramsay.


Cantona atashiriki katika kikosi cha wachezaji 11 maarufu kitakachoshirikisha wachezaji wa zamani na watu maarufu wakiongozwa na nahodha Usain Bolt.

Itakuwa mara ya kwanza kwa yeye kucheza katika uwanja huo tangu 2001.

''Ninarudi kuhakikisha kuwa mechi hiyo ya Juni 10 ndio bora zaidi na nataka mujiunge nami'', alisema raia huyo wa Ufaransa.


"Njooni tuweke historia katika uwanja wa OLd Trafford kwa mara nyengine ya mwisho''.

Atakabiliana na kikosi cha Uingereza kitakachoongozwa na mwanzilishi wa soka ya hisani Robbie Williams.
Atajiunga na wachezaji wengine wa zamani wa Manchester United akiwemo Phil Nevile na Edwin van der Sar.

Wachezaji wengine wa kikosi hicho cha dunia watakuwa Yaya Toure, Clarence Seedorf, Robert Pires , Jaap Stam na Patrick Kluivert.


Watakabiliana na David Seaman, Jamie Redknapp, Danny Murphy na Robbie Fowler kwa upande wa kikosi cha UIngereza.

Cantona ambaye alijiunga na klabu ya Manchester United kwa dau la £1.2m in 1992 - alifunga mabao 64 katika mechi 143 za ligi akiichezea Manchester United na kushinda mataji manne ya ligi ya Uingereza pamoja na mataji mawili ya kombe la FA katika misimu mitano.


mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu