CHELSEA YASHINDWA KUJIWEKA SEHEMU SALAMA KUCHEZA LIGI YA MABINGWA ULAYA MSIMU UJAO
Huddersfield Town wamejihakishia nafasi ya kusalia katika ligi hiyo kwa msimu ujao baada ya kwenda Sare ya kufungana goli 1-1 na Chelsea.

Kwa matokeo hayo ya Huddersfield, Swansea City inakuwa timu ya tatu kushuka daraja na kuunga na Stoke city na West bromwich Albion.

Na matokeo hayo yanaifanya Chelsea kuwa katika wakati ngumu kufuzu kushiriki michuano ya klabu bingwa ulaya.


Leicester City ikicheza nyumbani katika dimba la King Power waliwatungua Arsenal kwa magoli 3-1.

Manchester City wamezidi kuwa na msimu bora baada ya kuichapa Brighton kwa magoli 3-1 na kuweka rekodi ya timu iliyopata alama nyingi zaidi kwa msimu na timu iliyofunga magoli mengi zaidi kwa msimu wakiwa na magoli 105.


Tottenham hotspurs imejihakishia nafasi ya kucheza michezo ya klabu bingwa ulaya kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kupata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Newcastle United.

Leo unapigwa mchezo mmoja wa ligi hiyo Wagonga nyundo West Ham watakuwa wenyeji wa Mashetani Wekundu Man Unitedmzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu