BARCA YAZIDI KUNG'AA HUKU MADRID WAKIPOTEZA DHIDI YA SEVILLA


Barcelona imesalia na mechi mbili kuandikisha rekodi ya kutofungwa msimu mzima katika ligi ya La Lga baada ya kuicharaza Villarreal huku Ousmane Dembele akifunga mabao mawili.

Philippe Coutinho alifungua mfereji wa mabao baada ya kipa kupangua shambulio la Dembele huku Paulinho akifunga bao la pili.

Wakati huohuo nahodha wa Real Madrid Sergio Ramos alikosa mkwaju wa penalti ,akajifunga goli moja kabla ya kufunga mkwaju mwengine wa penalti huku Real Madrid ikipoteza kwa Sevilla 3-1.

Wissam Ben Yader aliiweka mbele Sevilla kabla ya Steven Nzonzi kufunga bao la pili kufuatia pasi ya Miguel Layun.

Ramos alijifunga kufuatia krosi iliopigwa na Gabriel Mercado na hivyobasi kuipatia Sevilla uongozi wa 3-0. Real ilijipatia bao la kufutia machozi kupitia Borja Mayoral aliyefunga kichwa kabla ya Ramos kufunga mkwaju wa penalti na kuipatia Real 2.

Real ambao walicheza bila nyota wao Cristiano Ronaldo itakabiliana na Liverpool mjini Kiev Mei 26.

Tukirudi katika uwanja wa Nou Camp, Lionel Messi alifunga pasi nzuri kutoka kwa Andres Iniesta.

Nicola Sansone aliisawazishia Villareal kabla ya Dembele kufunga mabao mawili mwisho wa kipindi cha pili.

Dembele alicheka na goli lililokuwa wazi kufuatia kazi nzuri ya Ivan Rakitic kabla ya kufunga bao lake la pili baada ya kupokea mpira kutoka nusu ya uwanja akawachenga mabeki kadhaa na kumpiga kanzu kipa Sergio Asenjo.

Iniesta alipatiwa heshima ya hali ya juu alipokuwa akitoka uwanjani muda mfupi baada ya kipindi cha pili kuanza .

Nahodha huyo wa Barcelona anaondoka katika klabu hiyo ambapo amecheza kipindi chote cha maisha yake ijapokuwa kuna ripti kwamba huenda anaelekea nchini China.

MZUNGUKO.COM


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu