ATHLETICO MADRID YAIKANYA BARCELONA KWA GRIEZMAN
Klabu ya soka ya nchin Hispania Athletico Madrid inasema kuwa imechoshwa na kero la Barcelona la kumnyatia mshambuliaji wake Antoine Griezmann, na imetaka mabingwa hao wa La Liga kuwa na heshima.


Akizungumza siku ya Jumatatu, rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu alisema kuwa alikutana na ajenti wa Griezmann mapema msimu huu


"Tumechoshwa na tabia mbaya ya Barcelona ," alisema afisa mkuu mtendaji wa Atletico Miguel Angel Gil Marin.


Marin aliongezea kuwa matamshi ya Bartomeu kuhusu Griezmann kabla ya mechi ya fainali ya ligi ya Europa kati ya Atletico na Marseille mnamo Mei 16 ilionyesha ukosefu wa heshima


Pia aliishutumu Barcelona kwa kuendelea kumshinikiza Griezmann msimu wote huu na kusema kuwa alimwambia Bartomeu miezi kadhaa iliopita kwamba tabia hiyo mbaya ni kinyume na maadili ya La Liga , wakati ambapo timu zote mbili zinapigania taji la ligi hii


mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu