GIGS ANENA JUU YA AFYA YA ALEX FERGUSONMeneja wa Wales Ryan Giggs anasema anatumai na anaomba meneja wake wa zamani Sir Alex Ferguson ataweza kupona uvujaji wa damu ubongoni.

Ferguson, mwenye umri wa miaka 76, bado yupo katika hali mahututi baada ya kufanyiwa upasuaji wa dharura siku ya Jumamosi.


Meneja huyo wa zamani alimruhusu Giggs wakati huo akiwana miaka 17 kucheza kwa mara ya kwanza katika timu ya Manchester United mnamo 1991 na alikuwa katika kikosi cha kwanza cha mechi 13 za Ferguson na kushinda mataji ya Premier League.

"Sasa ni wakati wa kumuombea na kutamaini kuwa atapona kikamilifu," Giggs alisema.


"Amekuwa na ushawishi mkubwa katika kazi yangu ndani na hata nje ya uwanja.

"Najua upasuaji ulikuwana ufanisi - lakini yeye ni mpanaji na hilo ndilo linalonifanya nikafikiria kuwa ataweza kupona."aliongeza Gigs


Mzunguko.com
Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu