LEBANON WAANZA KUPIGA KURA BAADA YA MIAKA 11


Raia nchini Lebanon hii leo, walionekana katika misururu mirefu ya foleni kwa lengo la kupiga kura kuwachagua wabunge wao baada ya kipindi cha miaka 11 kupita.

Mamlaka ya Bunge la mwisho iliongezwa mara mbili zaidi kutoka na vita vinavyoendelea nchi jirani ya Syria, na hivyo kuacha nafasi ya kufanyia marekebisho sheria za uchaguzi nchini humo.

Masuala kama ya rushwa,uchumi uliogubikwa na madeni kutokana na mikopo mingi, na changamoto nyingi za huduma za jamii ni baadhi ya mambo yaliyotawala harakati za kampeni


Nako nchini Tunisi, uchaguzi wa kwanza wa manispaa umefanyia tangu kupinduliwa kwa raisi Zine El Abidine Ben Ali mnamo mwaka 2011,kitendo kilichosababisha kutokea kwa vugu vugu la kudai demokrasia na utawala bora katika nchi za kiarabu na tangu wakati huo serikali za mitaa zilikuwa zikiongozwa na maafisa walioteuliwa na raisi.


Uchaguzi huo umeonekana kama fursa ya kuimarisha kipindi cha mpito kuelekea demokrasia ya kweli na kwa viongozi wa serikali za mitaa kuwajibika kutokana na huduma wanazotoa .


Zaidi ya watu milioni tano wa Tunisia watapiga kura hii ni kwa muujibu wa wachambuzi wa siasa nchini humo wanasema kuwa walio wengi hasa kundi la vijana hawatapiga kura kwa sababu ya kile wanachokiona kama ukosefu wa maendeleo ya kiuchumi.


mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu