Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

YONDANI ASIMAMISHWA KUITUMIKIA YANGA

May 3, 2018

 

 

 

Bodi ya Ligi Tanzania, imetangaza kumsimamisha beki wa Yanga, Kelvin Yondani kutokana na kuonekana katika video akimtemea mate beki, Asante Kwasi.

Mtendani wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura amezungumza hivi punde na kusema suala lake limepelekwa Kamati ya nidhamu baada ya kuonekana haliwezi kusikilizwa na Kamati ya Saa 72 iliyokaa.

 

 

 


"Kwa hiyo sasa tunamsimamisha hadi hapo kamati itakapokaa na kuamua kuhusiana na suala lake," alisema Wambura.

Katika picha ya video ilimuonyesha Yondani akimtemea Kwasi raia wa Ghana katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyowakutanisha watani wa jadi, Yanga na Simba ambao walishinda kwa bao 1-0.


Jambo hilo limeleta sintofahamu tangu kutokea kwake siku ya jumapili na hivyo wadau mbalimbali wa soka kulalama kwani kulikuwa hakuna hatua yoyote ya kinidhamu iliyochukuliwa dhidi yake

 

Yanga wapo ugenini Algeria kusubiria kucheza mchezo wao dhidi ya USM ALGER ya nchini humo katika hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barano afrika ngazi ya vilabu.

 

mzunguko.com
 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload