GODBLESS LEMA AKAMATWA TENA
Leo April 27, 2018 stori ninayokusogezea ni kumhusu Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema ambapo amekamatwa na jeshi la polisi na kufunguliwa mashtaka mapya kuhusu uchochezi kutokana ndoto aliyowahi kuota kuhusu Rais Magufuli.


Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema amesema kuwa Lema alihudhuria Mahakamani kwa ajili ya kesi iliyokuwa ikimkabili kuhusiana na ndoto alizoota miaka miwili iliyopita.


“Polisi Arusha wamemkamata Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema kwa kile kinachodaiwa “uchochezi”. Dhidi ya Rais kuhusiana na ndoto aliyowahi kuota” amesema Mrema


“Lema alihudhuria Mahakamani leo kwa ajili ya kesi iliyokua ikimkabili kuhusiana na ndoto alizoota miaka 2 iliyopita. Baada ya Mahakama kufuta kesi hiyo leo na kuachiwa. Polisi walimkamata tena na kumfungulia kesi upya kwa mashtaka yale yale” amesema John Mrema


MZUNGUKO.COMTufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu