WAANDISHI WA HABARI WAHUKUMIWA KWENDA JELA
Mahakama nchini Uturuki imewahukumu waandishi wa habari 13 jela kwa kuhusishwa na ugaidi, jambo ambalo limesababisha hasira duniani juu ya uhuru wa vyombo vya habari.


Waandishi hao wanaelezwa kuwa wafanyakazi wa gazeti la chama cha upinzani la Cumhuriyet ambalo limekuwa kinyume na serikali ya nchi hiyo kwa kipindi kirefu.


Waandishi hao walikamatwa baada ya jaribio la kupindua serikali liliposhindikana mwaka 2016.


,mzunguko.comTufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu