REAL MADRID YAINYOOSHA BAYERN MUNICHEN NYUMBANI ALLIANZ ARENA


Real Madrid ilichukua udhibiti wa nusu fainali ya kombe la vilabu bingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich katika mechi ya awamu ya kwanza kwa kujipatia ushindi katika uwanja wa Allianz Arena.

Mabingwa hao watetezi wanaojaribu kushinda taji hilo kwa mara ya tatu mfululizo walionekana kudorora katika safu ya ulinzi huku wakiwa na makali katika ile ya mashambulizi kabla ya Marcelo na Asensio kufunga katika kila kipindi cha mchezo.

Marcelo alifunga karibu na eneo la kupiga penalti na kusawazisha kabla ya Asensio kuongeza bao la pili baada ya Rifinha kufanya masikhara hivyobasi kuwapatia bao la ugenini.


​Mabingwa hao wa Ujerumani walikosa nafasi nyingi za wazi katika hatua ya mashambulizi, huku bao la mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo likikataliwa kwa kuunawa mpira huku ufungaji wake wa mabao katika kila mechi ya vilabu bingwa ukisitishwa.

Bayern sasa watalazimika kufunga mabao mawili Jumanne ijayo ili kuwazuia Real Madrid kufika fainali ya nne katika kipindi cha miaka mitano.Real wamekuwa wataalam wa kusonga mbele katika makundi hatua ya mtoano katika misimu ya hivi karibuni na ushindi huu ulikuwa mfano mzuri wa matokeo yao.

Tatizo lao la safu ya ulinzi lililowafanya kupoteza 3-1 dhidi ya Juve katika awamu ya pili ya robo fainali lilijitokeza tena katika kipindi cha kwanza na wangekuwa nyuma zaidi kabla ya Marcelo kupata bao.


Mkufunzi Zinedine Zidane alifanya mabadiliko baada ya kipindi cha kwanza akimtoa Isco na kumuingiza Asensio lakini mchi hiyo ikaendelea kama ilivyokuwa.

Hatahivyo Rafinha alifanya alipoteza mpira na kunaswa na wapinzani karibu na eneo la kati , Lucas Vazquez na Asensio waliupata mpira wakatamba nao kabla ya kumvisha kanzu kipa wa Bayern na kucheka na wavu kwa goli la pili.


Image captionWachezaji wa Bayern baada ya kulzwa na nyumbani na Real Madrid

Ronaldo hakupata fursa ya kushambulia katika mechi hiyo , ikiwa ni mara ya kwanza kwa yeye kushindwa kufanya hivyo katika kombe la vilabu bingwa tangu Mei 2017.

Alikuwa na fursa mbili ambapo alipiga nje kwa kichwa mbali na mkwaju uliotoka nje.


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu