MAPATO YA FACEBOOK YAONGEZEKA BAADA YA KASHFA

April 26, 2018

 

 

Wiki kadhaa zimepita baada ya kampuni ya Facebook ikabiliwe na kashfa ya matumizi mabaya ya taarifa binafsi za wateja wa mtandao huo zaidi ya Milioni 50 kulikofanywa na kampuni ya Uingereza ya Data Analytica iliyokuwa na uhusiano na timu ya kampeni yaRais Donald Trump mwaka 2016

 

Hatahivyo tofauti na ilivyodhaniwa, Facebook imeripoti kuwa mauzo ya kampuni hiyoyameongezeka kwa asilimia 50 tangu kashfa hiyo itokee na kutingisha kampuni hiyo.

 

Inaelezwa kuwa mapato ya kampuni hii yamepanda hadi kufikia Dola za Marekani bilioni 11.9 sawa na shilingi Trilioni 28.5 katika kipindi cha mwezi January hadi March mwaka huu 2018 ukilinganisha na Dola bilioni 8 miaka iliyopita.

Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Mark Zuckerberg ameeleza kuwa “pamoja na kukabiliwa na changamoto, biashara yetu imeanza vizuri mwaka 2018 na tunachunguza upya wajibu wetu”

 

MZUNGUKO.COM

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon