Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

KOCHA WA LIVEPOOL AOMBA MASHABIKI WAIHESHIMU AS ROMA

April 24, 2018

 

 

Siku ya leonchini Uingereza  kutakuwa na mtanange mkali wa mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya UEFA Champions League katika uwanja wa Anfield utakaozikutanisha timu za Liverpool ya England dhidi ya AS Roma ya Italia,  Siku ya jana kocha wa Liverpool Jurgen  Klopp aliongea na waandishi wa habari.

 

Kuelekea mchezo huo Jurgen Klopp akiongea na waandishi wa habari pia ametumia muda huo kuwaomba mashabiki wa Liverpool kuwaheshimu AS Roma na kuwanesha heshima kwa kutowafanyia fujo kama walivyofanya kwa Man City.

 

 

Klopp ambaye anaiongoza Liverpool katika mchezo kwanza wa nusu fainali ya UEFA Champions League toka 2008, anaamini mchezo dhidi ya AS Roma nyumbani utakuwa mgumu na asingependa kuona mashabikiwa wa Liverpool wakiwashambulia Roma kama walivyofanya katika game ya robo fainali kwa kuishambulia Man City.

 

Mzunguko.com

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload