Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

GARI LAGONGA WATU NA KUUWA 9,WENGINE 16 WAJERUHIWA

April 24, 2018

 

 

 

Watu tisa wameuawa mjini Toronto, nchini Canada baada kugongwa na gari la mizigo ambalo lilielekea katika mtaa wenye watu wengi. Wengine 16 wamejeruhiwa pia.

Mashuhuda wanasema kuwa dereva huyo aliendelea kuliendesha gari takribani umbali wa kilomita moja hivi.

 

"Lori hilo liliwagonga mwanamke na mwanaume.Hata hivyo baada ya kuwagonga watu hao dereva wa gari hilo aliendelea kuendesha gari hilo ambapo,mita chache mbele kulikuwa na miili mitano ama sita ikiwa chini.Na inavyoonekana dereva alikuwa akiyumbisha gari nje mara ndani ya mtaa huo,ilikuwa ni jambo la kutisha." Diego De Matos

 

"Kuna ushirikiano wa kutosha kwa Polisi,katika kuchunguza jambo hilo,na tutatoa majibu ya hili kwa umma.Lakini kwa sasa hakuna taarifa zozote kwangu kuhusiana na chanzo ama lengo la tukio hili.'' Ralph Goodale

Kumekuwa na matukio ya magari makubwa kutumiwa na magaidi kusababisha vifo katika maeneo yenye mikusanyiko,baada ya mamlaka za usalama kudhibiti njia za magaidi hao zilizooeleka.

 

Matumizi ya magari makubwa ya mizigo,ni mfumo mpya ambao umekuwa ukitumiwa na magaidi kutekeleza azma yao kufuatia kubainika kwa njia zao zilizo mara zote.

 

mzunguko.com

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload