CAG AMWAMBIA RAISI HAKUNA TRILIONI 1.5 ILIYOPOTEA,Leo Mheshimiwa Rais wa Jamhuri Dr. John Magufuli amesema alishangazwa kusikia kuna TRILIONI 1.5 imepotea na alipopata taarifa hizo alimpigia CAG, Prof Assad kumuuliza mbona katika ripoti aliyomsomea Ikulu hakuona kiasi hicho.


“Niliposikia Serikali imeiba TRILIONI 1.5 nikampigia CAG na kumuuliza mbona katika Ripoti uliyoisoma hapa Ikulu sikuona kuwa kiasi hicho kimepotea?, akajibu kuwa hakuna kitu kama hiko, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha nae akasema hakuna” -Rais Magufuli


Rais Magufuli alipowauliza CAG, Prof. Assad na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Doto James wamesema mbele ya JPM kuwa hakuna fedha Trilioni 1.5 zilizoibiwa na Doto James akasisitiza kwa kusema hazina ‘wako salama’mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu