LUKAKU RASMI MIKONONI MWA JAY Z

April 20, 2018

 

 

 

 

Staa wa Man United na timu ya taifa ya Ubelgiji Romelu Lakaku leo ametangaza siku ya juzi kama siku nzuri zaidi  katika maisha yake ya soka, Lukaku ametangaza rasmi kusainiwa na Roc Nation Sports Agency ambayo inamilikiwa na staa wa muziki wa Marekani Jay Z.

 

Baada ya kusaini mkataba huo Lukaku mbele ya mama yake mzazi sasa atakuwa akisimamiwa na Roc Nation Sports Agency katika shughuli zake zote za kisoka kama dili za matangazo ya biashara.

 

Lukaku ambaye amesaini dili hilo akiwa New York Marekani ndio anakuwa mchezaji wa kwanza kutoka Ligi Kuu England kupata nafasi ya kuingia mkataba na Roc Nation Sports Agency inayomilikiwa na rapper Jay Z.

 

mzunguko.com

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon