Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

JALADA LA MAUAJI YA AKWILINA LIMEFUNGWA RASMI,WATUHUMIWA WAACHIWA HURU

April 20, 2018

 

 

 

 

 

Leo April 2018 Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Biswalo Mganga amesema, jalada la kesi ya aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini amelifunga rasmi.

 

Akizungumza na waandishi wa habari Ikulu ameonya watu wanaovunjua amani kutofumbiwa macho wakiwamo waandishi wa habari.

 

Amesema jeshi la polisi linapotumia nguvu kuzuia maandamano, haliwezi kushtakiwa au hata kukitokea vurugu na kusababisha mauaji huwezi kulishtaki jeshi.

 

“Katika maandamano yale ya watu zaidi ya 200, huwezi kubaini nani amehusika na kumpiga risasi Akwilina na mwili wake haukutolewa risasi yoyote.” -Biswalo

 

Alipoulizwa kuhusu askari waliokamatwa baada ya kutokea kwa tukio hilo, Biswalo amesema, “kama jalada nimelifunga, kwa hiyo askari wale nao wameachiwa huru hawana hatia.”

 

“Niseme tu kuwa, mimi sina chama cha siasa, si mwanasiasa, kwa hiyo sitamvumilia mtu awe mkubwa wala mdogo, nitamshughulikia.” -Biswalo

“Na wanaosema wataandamana, waambieni wasifanye hivyo kwani wakiandamana watakwenda kuwasilimulia familia zao,” -Biswalo

 

mzunguko.com

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload